Tanzania emblem

Ofisi ya Rais

Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa

Building photo

Mafunzo ya watunza Kumbukumbu-mhimili wa Mahakama


KATIKA maboresho mbalimbali ya huduma zake, Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya jitihada kadhaa kuhakikisha huduma zake zinakuwa bora zaidi. Katika makala haya, tutaangazia maboresho katika utunzaji bora wa kumbukumbu ndani ya mahakama. Katika mhimili wa mahakama, suala la utunzaji wa kumbukumbu ni muhimu kwani kwa asilimia kubwa, mahakama inafanya kazi kwa kutumia kumbukumbu zinazohifadhiwa kimaandishi. Kwa umuhimu huu, masjala ndiyo kitovu kikuu katika uendeshaji wa mahakama kwa kuwa baadhi ya kumbukumbu huhifadhiwa huko. Katika mahojiano maalumu na Mkurugenzi wa Kumbukumbu, Mahakama ya Tanzania, Malimo Manyambula anasema neno kumbukumbu linatokana na neno la Kilatini lijulikanalo kama ‘recordum’ ikiwa na maana ya ushuhuda wa shahidi (testimony of witness). Manyambula anazidi kulielezea neno kumbukumbu akisema ni taarifa ya kimaandishi inayopokelewa au kuzaliwa na taasisi husika ili kusaidia taasisi hiyo kutoa uamuzi sahihi na kwa wakati mfupi iwezekanavyo.