Tunafanya Nini
- Kusimamia na kuratibu utekelezaji na uzingatiaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za utunzaji Kumbukumbu na Nyaraka katika Taasisi za Umma.
- Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Kuwaenzi Waasisi wa Taifa Na. 18 ya mwaka 2004 katika kukusanya, kutunza na kuhifadhi Kumbukumbu na vitu vya Waasisi wa Taifa letu (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume).
- Kuweka mifumo ya utunzaji Kumbukumbu na Nyaraka katika Taasisi za Umma ili kuongeza ufanisi na tija katika utoaji wa huduma Serikalini;
- Kutoa ushauri juu ya utunzaji bora wa Kumbukumbu na Nyaraka pamoja na kuratibu mipango ya kutunza na kuhifadhi Kumbukumbu muhimu (vital Records) katika Taasisi za umma;
- Kuweka na kusimamia viwango vya utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka katika Taasisi za umma;
- Kukusanya na kuhifadhi Nyaraka muhimu ili kulinda historia na urithi andishi wa nchi yetu;
- Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa miongozo ya kutunza Kumbukumbu na Nyaraka katika Taasisi za Umma;
- Kuandaa na kuratibu mipango ya kudhibiti na kukabili majanga (disaster preparednes and recovery programs) yanayoweza kuharibu Kumbukumbu na Nyaraka zilizohifadhiwa na Idara;
- Kufanya tathmini (appraisal) ya majalada tuli (majalada yaliyofungwa) ili kutambua majalada yenye umuhimu wa kudumu kwa ajili ya kuyahifadhi na kubaini yasiyo na umuhimu kwa ajili ya kuteketezwa kwa mujibu wa Sheria;
- Kuhifadhi Nyaraka kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kurahisisha upatikanaji wake na kulinda nakala halisi;
- Kukusanya, kutunza na kuhifadhi Kumbukumbu na vitu vya Waasisi wa Taifa; ili kuhifadhi na kudumisha fikra na falsafa zao kwa kizazi cha sasa na vijavyo; na
- Kuhamasisha Umma ili uweze kufahamu na kutumia huduma zitolewazo na Idara.