Kituo cha Taifa cha Kutunzia Kumbukumbu Tuli chajengwa Dodoma
Kituo cha kutunzia kumbukumbu Tuli (Records Centre) ni jengo/mahali panapotumika kutunzia kwa muda kumbukumbu zilizofungwa, kwa
usalama na gharama nafuu, wakati zikisubiri kufanyiwa tathmini ya kujua umuhimu wake na hivyo kuamua kuendelea kutunzwa, katika kituo, kuhamishiwa sehemu ya Nyaraka au kuharibiwa kwa kumbukumbu zile zitakazooonekana hazina umuhimu wa kudumu.