Tanzania emblem

Ofisi ya Rais

Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa

Building photo

Neno la Ukaribisho

Bw. Firimin Msiangi
Mkurugenzi

Mnakaribishwa kwenye Tovuti ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa. Kumbukumbu na Nyaraka ni nyenzo muhimu katika utendaji kazi Serikalini na Taasisi zake. Bila ya kuwa na kumbukumbu sahihi hatuwezi kujua tunakotoka na tunakokwenda na hivyo kushindwa kufikia maamuzi sahihi kwa wakati. Kumbukumbu hutumika kama kielelezo katika uwajibikaji na ni nguzo muhimu katika Utawala Bora. Ili Serikali iweze kufikia lengo hilo na kuwezesha umma kujua mwenendo wa Serikali yao, lazima kuwe na kumbukumbu zinazotunzwa vizuri na zinazopatikana kwa urahisi. Kukosekana kwa taarifa sahihi na kwa wakati unaofaa kunaweza kuwafanya Watendaji wa Serikali kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa maamuzi au kutolewa kwa maamuzi yasiyo sahihi na yasiyokidhi matarajio ya wananchi. Aidha, ukosefu wa kumbukumbu hutoa mianya ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka na hata kuchelewesha au kuzuia haki kutendeka. Kasoro hizi huchangia sana katika kuzorotesha maendeleo ya uchumi wa Taifa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu Serikali yao na Taasisi zake.

Ninatoa wito kuzitunza na kuzithamini Kumbukumbu zetu,Tukumbuke kwamba,Nyaraka ni urithi wa Taifa.